Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mheshimiwa Rachel Kassanda leo tarehe 28.01.2019 ameitembelea Shule ya Sekondari ya Inyonga na kukagua Madarasa mawili yanayojengwa ajili ya kumaliza changamoto ya Madarasa mawili yanayojengwa baada ya hao wanafunzi kukosa madaras awali! Mheshimiwa D.C ameagiza Ubao wa kuandikia na Madawati yote kuwekwa Kwenye Madarasa hayo mawili ili Masomo yaendelee! Pia Mheshimiwa D.C ametumia muda huo kuongea na Walimu wa Shule hiyo ambapo amewataka Walimu hao kujituma zaidi ili Mwaka ujao ufaulu uongezeke zaidi! Pia Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya aliweza kunywa Soda Walimu wa Shule hiyo! Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi pia wamewaahidi Walimu watakaofundisha na kufanikiwa kufaulisha wanafunzi wao kwa kupata Alama ‘A’ Kwenye Somo atapata Motisha ya Tsh 50,000/= kwa kila ‘A’! Aidha Walimu pia wameaidi kufundisha kwa bidii!
Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele
Anuani ya Posta: S.L.P 686 MPANDA
Simu: +255759023788
Simu ya Kiganjani: 0759023788
Barua pepe: ded@mleledc.go.tz
Hakimiliki ya @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Hakizote zimehifadhiwa